UNGANA NASI
Tunakutana mtandaoni mara tatu kwa wiki. Jumanne, Jumatano na Jumamosi

RATIBA YA SALA
SIKU YA JUMANNE: SAA 3 USIKU MAJIRA YA MASHASHARIKI ( MAREKANI)
SIKU YA JUMATANO: SAA 3 USIKU MAJIRA YA MASHARIKI ( MAREKANI)
SIKU YA JUMAMOSI: SAA 4 ASUBUI MAJIRA YA MASHARIKI ( MAREKANI)
PIGA SIMU KWENDA NAMBA +1-585-1818

MAFUNZO YA BIBLIA
Tusomapo maandiko, Mungu huzungumza nasi na tunabadilishwa. Tunapojifunza Biblia pamoja, Mungu anaahidi kujifunua, kutufundisha jinsi ya kumtii, na kutuonyesha jinsi ya kupendana. Tunapobadilishwa na kuwa kama Yesu, familia zetu, mahali pa kazi na jumuiya zitaathiriwa milele.

MAFUNDISHO YA KANISA
Mafundisho ya kanisa hutoa mfumo mpana wa kuelewa imani, maadili, na jukumu la Kanisa ulimwenguni. Wakatoliki na wasio Wakatoliki wote wanaalikwa kuja kujifunza mafundisho ya Kanisa na kundi la Upya Kiroho, karismatiki katoliki.
MAOMBI KWA MATENDO NI UPENDO, UPENDO KWA MATENDO NI HUDUMA.” – MAMA TERESA
Ni furaha yetu kushiriki injili kwa kuwasaidia wale walio na uhitaji. Tunashirikiana na vikundi vingine vya hisani kote Afrika Mashariki ikijumuisha Tanzania, Uganda, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, Burundi kusaidia wale walio na mahitaji.

“Ninyi, wakarismatiki, mmepokea zawadi kuu kutoka kwa Bwana. Kuzaliwa kwa harakati zenu kulikubaliwa na Roho Mtakatifu kuwa ‘ mkondo wa neema katika Kanisa na kwa Kanisa’. Huu ndio utambulisho wenu: kuwa mkondo wa neema.”
Pope Francis












